adam shule kongwe - kurasa zilizokosekana lyrics
verse 1:
africa ni taifa sa kwa nini waigawanye
wao wametukuta watakuaje wafalme
hawa wajinga walijivisha unadhifu
kisha viongozi wetu wakawaita ma chief
wauaji kama leopold kongo
mamilioni ya watu walif+kiwa kwenye udongo
sambamba na ukatili kama kukatwa mikono
na kutumikishwa hakujafikaga kikomo
migodi ya south vibarua ni wazawa
licha ya kazi ngumu walichukua roho zao
almasi na dhahabu zenye damu
mateso mbalimbali ya mababu kwenye mashamba
++++++mi napata moto kwa hakika
hasa inapofika, siku ya mtoto wa africa
kaburu kutafuta uhuru kwani kosa
nalilia watoto wa kizulu na kikhosa
verse 2:
wanatuona vibomba hawa jamaa
naskia eti papa alishaomba msamaha
nilishangaa, huo ni upendo wa wapi
mnajua mlipoteza wazalendo w+ngapi
itabadili nini, kivipi
mtatuambia nini saivi
kama mama africa alidhalilishwa vilivyo
kwenye human zoo watoto walilishwa hadi ndizi
hamuandiki, mnatuongopea achen fix
badala yake mnatuletea mafeminist
na hadi leo mmebakisha vinasaba
mkaleta democrasia kuzalisha vibaraka
wa umoja wa mataifa au umoja wa mataita
boda za bongo hao masoja wataisha
mnawaua wakati nyie mnashinda ndani
na mkuu anajisifu kusema w+n+linda amani
verse 3:
tazama mauaji ya wenyewe kwa wenyewе
power ya waasi kusimama vifua mbele
silaha za kivita na kibaiolojia
dini kutugawa hadi tunajichukia
wanapеana vijiti toka karne
hii kalamu ni zaidi ya mashine ya bomba nane
na popote napowafuma namimina
sijaganda mawazo ka watumwa wa kifikra
usiniulize kwamba nani namkolea
au nani noma kati ya mmarekani na mkorea
huwezi nikuta namshabikia trump
hawa walete acha waikanyagie track
mi kioo cha jamii i let the freedom ring
siwezi sifia wasenge kama kim jong ill
iko wazi watasiliba ninavyotukana
kitu wanachosifu ni jinsi china inavyotufanya
Random Lyrics
- catboot - rap quoi québé lyrics
- owen adamcik - see the girl lyrics
- freezepop - tenisu no boifurendo (kodomo remix) lyrics
- lastvel - light it up lyrics
- ruby lewis - praying patience lyrics
- brusco - mi accendo lyrics
- negative xp - waiting (demo) lyrics
- iann dior - valentine's day in hell lyrics
- scorp tmk - zum zum lyrics
- over the moon - hey boy lyrics