cash donta - who dat lyrics
word to the wise, a runner must run with dreams in his heart not money in his pocket, cash doro cash donta, ommy runner m-ss town in the house, we run this shit ni**a, dirty south check it out
verse 1(cash donta)
“bad news” ah! ndivyo walivyomwita
the real mc, mchawi wa bars kumi na sita
“abracadabra” microphone magician aliisadikika
ilionekana ni ajabu kwa kila irabu aliiyoandika
“the king of mic” zaidi ya laki wali-like kumwita
alijua zaidi ya kuchana instrumental ilipokita
fire flame spitter daima frontline ka militia
ndani ya cypher alitisha kwa sk!llz fake mc’s walikwisha
aliamini fata misingi ili uwe king kama msindi
akasadiki nguzo tano ndo tumaini la ushindi
hakuwa na coin ila tulijua atakuwa icon wa hip hop
na daz wazzup, uzinduzi wa camp ukamwashia lamp
akajump, na kujikuta kwenye limelight
mfadhili akampa record deal, waka-sign contract
na money is power basi mzawa alivyozipata contact
track alizo release[kwenye media] zikaleta impact!!
chorus 1
who dat? who dat? the boy right here
microphone magician aliyeziteka zangu hisia
kwa kuirudisha hip-hop kwenye chati ya milenia
kila nafsi iliamini pia huyu ndo “returned messiah” *2
verse 2
akairudisha hip-hop kwenye zama za chemsha bongo
kipaza kikapata shujaa wa jah, aliyejivika usongo
hakuendekeza madongo, japo ali-criticize uongo
na ku-dis kimtindo jamii itoke kwenye korongo
hakuwa mtu wa longo longo, daima straight to the point
aliwachana hadi ma mp wa dom, wa- legalise joint
“real hip-hop is not on the radio” aliwaambia ma-promota
waibue vipaji kila siku mtaani anazaliwa nyota
hakusita kueleza alivyosota kwa kutupa historia ya alipotoka
wengi wana-fake, anairudisha hip-hop ka enzi za wana-choka
alikuwa cautious, makini pia conscientious
harakati hakubaki nyuma ali scan mpaka virus
wengi tulimpenda sababu mchizi alikaza
jioni tulijikusanya ki-stone, ili atupe ladha
freestyles na acapella one after another
ilikuwa ni zaidi ya hip hop darasa iliyonipatia mwangaza
chorus 2
sikia, story ya the boy right here
aliechomoza juu ya dunia akaiunganisha hip-hop ka familia
kila mpendwa alimwita “dear” tumaini kwa kila aliefatia
but real hip-hop never change, sidhani alizingatia
verse 3
wanasema its easy kutoka ngumu ku-mantain
nahisi huyu jamaa alikuwa in the same train
akasahau, jinsi elimu dunia ilivyom-train
akaanza kuimba funny songs kwa lengo la ku-entertain
d-mn, but things will never be the same
baada ya kulewa umaarufu si ndo akapagawa na fame
hakukumbuka mbali alipotoka, it was only a dream
na reality ndo inatamba, huwezi ku-act kama film
kwa shobo za vicheche wa mtaa akajiona sukari ya warembo
akajiita “mungu wa rap’ kisa battle alikalisha matembo
skendo zikampunguzia upendo, waliompenda wakamchoka
“mbona ana mikato ya kichoko?’ huyu hawezi kuwa wa kufoka
akaanza kuji-cream
cocaine ikageuka stimu
akapotezea ladha adimu
kwa kushobokea mziki wa mainstream
sponsor akavunja mkataba akabaki anatangatanga
sasa ni zaidi ya miaka saba na eti bado anajipanga!!!!!
chorus 3
sikia, story ya the boy right here
alieyafata ya dunia baada ya kutekwa na rupia
akajivua uhalisia ili ateke soko huria
but real hip-hop never change tayari kashafulia
outro
Random Lyrics
- braza - exército sem farda lyrics
- i fight dragons - save world get girl lyrics
- gypsy & the cat - naomi lyrics
- red l'alerte - romeo echo delta (schizofreestyles v) lyrics
- assassins - new york 2015 lyrics
- louis vierne - la cloche fêlée lyrics
- chief keef - swerve lyrics
- foggieraw - kyrie w/jayizms & masego lyrics
- 2scratch - superlife lyrics
- neven ilic - tengo que dejarte lyrics