dizasta vina - fallen angel lyrics
yoh
.. wanasema nilipenda bila tija, kwamba sikutaka kujifunza sikutaka tiba. nilikupenda na mtaani ilikuwa shida. nilikosana na watu maana nilikutaja kila mida
niligombana na wana uliposema nipunguze marafiki, ulihisi wengi wao wa nafikiria. ukasema niache muziki, nikaacha nikatafuta kazi ilimradi nipambane na dhiki. nikaona shega, kama kuna boya yeyote atanilaumu…..yamkini bado haj-penda. niliitika uliponita, nilifika nikakusikiliza na kila uliponituma nilikwenda
kama kupenda ilikuwa ajabu, nadhani hata ile kukonda ilikuwa sababu. ilikuwa kufanya maamuzi si jasiri, ila kwa sababu yako wala sikujiuliza mara mbili
kisa wewe, nikabuni kila mishe. nikapigana mpaka na kikundi ili nikuridhishe. nilikuwa mwoga nielewe, ila nilijipa moyo kuwa chochote kinawezekana… kisa wewe. niliamua nikupende bila ‘doubt’, nilisimama kila nilipoulizwa ‘nika-shout’. sikuogopa ugonjwa wala mauti. kwa sababu yako, nikakamatwa boda kule sauzi
nikuk-mbushe, shule nilikuwa king kwenye “dorm fights” ila nikapigwa na jamaa kwenye ’prom fight’. mahusiano yetu yalini-cost, kuna kipindi nilikosa dili nikazama mgodi
naumwa mama, hizi shida zipo. mama yako alipata ajali, nikatoa figo. nilikuwa nina mafua nakakuhitaji kama chafya ili nitoe. nilikupenda mpaka ukanigharimu afya
ulijua kuwa ninapenda hip hop lakini ikabidi nijue reggae. sikuwa tozi lakini nikajua chepe. nikazijua tembe. kichwa kilipokuuma, nikazama kutafuta (ni mapenzi na sikuwa bwege)
nilijitosa kuwa usafiri, nikufikishe. niliamua kuwa hata mwizi, nikuridhishe. kaka zako walipanga dili ili waniue, wakaishia kuniumiza nikakanda mwili
nilikupenda peke yako, sikujua mingo. kuna kipindi uliniweka kwenye matatizo, kwenye vikoba ulikopa hela mpaka nikakamatwa mimi nikafungwa jela mwaka. sikusoma, na sio kwamba nilitaka kufa na mali. ni kwamba sikutaka uteseke ndio maana nikakupa nyumba na gari. dili zikab-ma na tarehe za kulipa zikatimia…wadeni walipokuja, nilikimbia
nilipambana sana bado nikakosa dili. nikasafiri nikaenda kwa mganga ili niwe tajiri. sikupenda mwenzangu ufuturu njugu, nikavuka ukuta mpaka nikaanza k-mkufuru mungu
ndugu walinikimbia, nakili. nadhani walihisi zimenikimbia akili. walidhani ilikuwa ‘simple’ kuniasa. walifikia kusema nakupenda wewe kuliko ‘mother’
dah! nikavunja miiko, mpaka nikabadili dini nikawa mkristo. nilihadaa kufa, tulikosa mboga nikagaa gaa na upwa
ulipenda kupendeza, kugeza mitindo ulipenda kuongea kiingereza. nikakulipia shule, ulifanya madudu. nikakubali ili usome mimi nibaki mb-mb-mbu
nilipigana kila shari ilipokuja. nilizuga mi ni mwalimu kwa baba’ako. nilifulia wakaniita mcmugga, na mtaani nikawa adimu kwa ajili yako
“nilitaka uwe mke”, ni habari. nilitamani nikupeleke nje ya sayari. kuna muda nilisanda nikazama kila chaka, sikuogopa nge ni hatari
kwa yangu hiyari nikawa pusha. nilijifanya dalali nikauza gari na nyumba. mentali, sikungoja zali kunikuta. mali ulipofuja zote nikaenda mbali kutafuta
ulitamani rasta, nikasuka. ulitamani shamba na duka, ulitamani khanga nikakupa. sikuogopa nilikudaka ulipoanguka
washikaji walisema naoa lawama, nilifunga vioo tukafunga ndoa ya gharama. kazini nikabeba pesa kwakuwa nilikuwa ‘cashier’, nikakata tiketi twende ’honeymoon’ philadelphia
sikukwambia haya yote tangu mwanzo kwa kuwa sikupenda uteseke kwa mawazo. nilikulea ka baba’ako, sio mimi yalikuwa ni mapenzi juu yako
nilishiriki magendo, (mpaka kuua) nilitaka kuwa mjeda nikashiriki depo. nilitamani kukuoa kiukweli ndio maana muda wote huo hatukushiriki tendo
sikuibuka kilingeni, nikafunga ‘decoder’ na ‘subwoofer’ sebuleni. kuna kipindi nilik-mbwa na madeni ili upate saluni, nikajenga nyumba uf-kweni
nitapunguza vipi machungu? nilikosa nini kwa mungu. umekufa sikuoni tena getoni
umeniacha, mola akulaze pema peponi. amen
Random Lyrics
- kongehuset - nu går den vilde skattejagt lyrics
- cadelis - caos no laos lyrics
- wolfadvice - stevie (remix) lyrics
- parson james - oh love lyrics
- guccc - mood swings lyrics
- princess bri - no masters lyrics
- dana vaughns - rough rider lyrics
- smutny buni - 1999 / szlifuje lyrics
- i supremi - due ali lyrics
- ac.jr & brady james - find myself lyrics