dizasta vina - hatia iv lyrics
“jasiri john….. aliyaangalia maisha yake
hakuona jinsi angeweza kuishi bila jane
msichana anayempenda
licha ya kuzongwa na umasikini
alijitahidi k+mpa jane mahitaji madogomadogo kadri alivyoweza
lakini alifahamu shubiri ya kusubiri kupendwa huku anafahamu kusubiri kupendwa ni matumaini yanayoumiza. kama wanavyosema, mtafutaji hachoki akichoka kashapata….aliendelea kungoja”
ah! sikuwa na zali sikuziamini ndumba
sikuwa na mali za kufuja
nilijitahidi kuuza mitumba kufuga mipunga
ili siku nimpe gari nimpe nyumba. nilishindwa…
niliishia k+mpa chai, ‘chipsi’ mayai na ‘vocha’
nywele za kimasai na mkoba
pesa za magauni, majuba na viatu vya kuzuga
nilimpa muda ila bado haikutosha, kwani…
nilipomwambia nampenda hakujibu
akaweka moyo w+ngu maumivu
na mtima w+ngu akauweka ‘solemba’
nikaapia kuwa sitakuja kupenda ‘forever’
ah! nilimpa upendo nilimpa sifa
niliweka mitego ya faida, haikuwa shwari
nikabadili mwenendo wa maisha
niliweka malengo sikutimiza, hakunikubali
alikuwa na ndoto kubwa kushinda mimi
alikuwa na misimamo kuipita dini
aliniambia ameomba nije kuokota utajiri
amengoja sana na sasa amechoka kusubiri
“john alifahamu hali ya jane, kuwa jane alizaliwa kwenye
familia masikini, na aliuchukia mno umasikini. alifahamu umasikini ulivyochukua uhai wa mama yake kipenzi, aliyefariki kwa kukosa matibabu. aliifahamau nadhiri aliyoiweka jane ya kwamba hatokubali tena kuishi kwenye maisha ya kimasikini, nadhiri iliyo mweka john njiapanda”
ah! sikuwa na hali ya kuikosha roho yake
nilimwacha aende aufate moyo wake
alipata bwana wa kizungu magharibi
alimwahidi kuishi maisha ya ndoto zake
nilipata uchungu niliishia kuhamaki nilitaka nijiue
nilitaka nimzuie abaki nikak+mbuka
ukipenda ua haulikati unaliacha likue
duka langu nilifunga biashara niliacha zote
uchumi uliyumba kwa maana nilianza pombe
niliumwa bado kidogo moyo uzime
nilimfanya ndoto k+mbe naye ana ndoto nyingine
alisema anakwenda jiji la miami
hakuna alichowaza zaidi ya kuishi kifahari
kamtumia picha na ‘mchizi’ kazikubali
na yupo tayari k+mlipia gharama za safari
aliondoka na kipande kimoja cha mwili
nilikonda nilipata ugonjwa wa akili
haikuwahi kupita hata sekunde nisilie
nilitamani mpaka ardhi ipasuke niingie
“jane alipoondoka alimwachia john kidonda kilichochelewa sana kupona
na yeye akaweka nadhiri ya kutojihusisha na mapenzi tena maishani mwake. alikaa kwa muda mrefu bila mahusiano. lakini…
hakuna daktari mzuri kama muda, john alipona maumivu na aliirudia hali yake ya kawaida”
ah! muda ukaenda nitapata ‘mwanamwali’
nikamwomba awe mwenza wa maisha akakubali
nikamvisha pete nikalipia mahari
sik+mpenda lakini nilijifunza k+mjali
aliuliza kama nampenda, nilimjibu
sikutaka kuweka moyo wake maumivu
sikutaka kuuweka mtima wake solemba
kiasi aseme hatakuja kupenda ‘‘forever’’
ah alinik+mbatia nikamfunga kwa ishara
akanikabidhi tunda nikala
akaniamini tukajuana nikapanga k+mwoa
akaidhisha na tukaanza na mipango ya ndoa
“wakati karne ya 21 inaingia, john alikuwa ni miongoni mwa
vijana waliokuwa ‘fascinated’ na ukuaji wa teknolojia ya mitandao ya kijamii. alijiunga na dunia hii mpya, mara kadhaa alikaa kwenye ubaraza, akiangaza simu yake. akipapasa kila kitufe, ndipo siku moja akapata ujumbe kutoka kwa jane”
“habari naamini u bukheri wa afya
unaendeleaje maisha na huyo mpenzi wa sasa
.nashukuru nahema ughaibuni si kwema
nakiona cha mtema mpaka naona ni heri nikafa…
ah! maisha niliyowaza yote ni uongo
nauzishwa madawa nalazimishwa ngono
nafungiwa ndani kama mtumwa ufungwani
roho yangu rehani kiasi sasa naitamani bongo
ukubwa umekuja kunisafisha jicho
ndoto imeisha na taswira imenionyesha sivyo, ah
naomba unifate uniondoshe kwenye hichi kifo
na hii namba ya msamaria atakueleza nilipo”
sherehe ilikuwa na mipango madhubuti
kabla mimi kuichukua michango ya harusi
nikatoroka ughaibuni kufuata hisia zangu
kwenda k+mfata njiwa w+ngu mahususi
nilivuka majangwa na majabali
sehemu ya safari anga sehemu nyingine bahari
niliacha kila kitu nyuma upendo na huruma vilinijaa
penzi likanipeleka mbali
“john alifika ughaibuni, akamtafuta msamaria aliyetambulishwa na ujumbe, msamaria akamwelekeza njiwa wake alipo, na nikweli… hapakuwa pema”
nikakutana na bopa la kizungu
lenye sura ya kuichachisha mboga kwenye chungu
kiko kwenye mdomo,tatuu kila kona na wapambe
pamoja na vishoka wenye mtutu
sio siri alizungukwa na wasichana wengi
sikujua umri walikuwa wadogo ka’ “madent”
baadhi walikuwa uchi wanahesabia “chenchi”
wengine masaji huku wengine wanamchezea nyeti
“masikini john, alidanganya kwa kujitambulisha kama kaka kwa jane, akimsihi yule mafia amruhusu aondoke na jane wakaanze maisha mapya, lakini… paliposhindwa shoka wembe hauwezi tamba. kwa kuzidiwa na uoga wa kuuawa…jane alimkana john kwa kusema hamjui…”
hata nilipomuuliza kama ananipenda hakujibu
akaweka moyo w+ngu maumivu
nilijua hawezi kufa kwa sababu hakunipenda
na ni rasmi nikapoteza shilingi kwenye msitu
nilikiambia kifo kama unakuja njoo
maana sikuwa mtu ilishakufa roho
sikuumia kama alivyoniumiza yeye
kwahiyo sikujali jinsi nilivyoteswa na wale mbwa no
aliambiwa ambusu bosi hakubisha
alipewa bunduki hakusita
aliishika risasi akaiingiza
akaambiwa anipige kwenye kichwa
john alikuwa ni jina jipya la wahanga wa upendo wa dhati, vipofu wa mapenzi, wajinga wa mahaba…
john alikuwa romeo kwenye romeo and julieth, alikuwa samson kwa delilah kwenye wahuk+mu wa agano la kale, alikuwa jack kwenye titanic, fred weasley kwenye harry potter..
john alituk+mbusha kuwa upendo ni sadaka, sadaka ya muda na pesa, alituk+mbusha upendo ni sadaka ya damu
john, alipoteza uhai akiwa kwenye safari ya kutafuta upendo wa mtu aliyemhusudu na
jane alipoteza amani na thamani yake kama mtu akiwa kwenye safari ya kutafuta utajiri aliouhusudu
hatia iko wapi?
Random Lyrics
- элина чага (elina chaga) - отпустить (otpustit') lyrics
- antza - home - acoustic version lyrics
- scarlett - where i'm from lyrics
- terra lightfoot - it's over now lyrics
- bedoes & lanek - city boy :* lyrics
- giag700 - con me lyrics
- alpha wann - apdl lyrics
- drug flash - я не один (i'm not alone) lyrics
- katy kirby - cool dry place lyrics
- southside hoodlum - picture me rollin lyrics