dizasta vina - hatia v lyrics
yeah
nilimfahamu baba alikuwa jasiri
aliondoa utando ulipodandia kuta
alitoa nyoka makatili alipambana na
majangiri walipovamia nyumba
aliweka paa juu vichwa
hatukuogopa baa la njaa tulishiba
niliona wengine nguo za kuvaa zimechanika
wakati kwetu nyuso ziling’aa migongo ilifunikwa
radi ilipiga wala sikujali
maana baba alikuwa simba kwenye msitu mkali
wapo waliozijua sifa zake j+po
mtaani halikuwika jina lake
halikuandikwa bali
waliona poa ilikuwa juk+mu lake
mwanaume jasho kutoa ndio huk+mu yake
ajali ya kisu iliondoa ngozi
sik+mwona akitoa machozi
nilimwona kama role model
alikuwa shupavu hakuwa na roho ndogo
mara chache alianguka ali+score zero
alipambana upya kama war hero mdogo mdogo
maisha yake yalikuwa ni adventure
alikuwa ni handyman carpenter painter
alinijuza aliyoshuhudia kwa macho
maana aliisafiri dunia enzi zake kama vasco
alikuwa so gentle
alimpenda mama kupita maelezo
watu walijadili nini maana ya upendo
waliunda dhana mi niliiona maana kwa vitendo
huh
ugonjwa uliingia mama aliugua maradhi
homa ilivamia ghafla kupumua kazi
baba ali+suffer hospitali kadha wa kadha
changamoto afya kupigania zikafungua jamvi huh
hali ilileta mtiti
hakuipata nafuu ugonjwa ulimweka kingi
baba aliwapa waganga wakuu pesa nyingi
mixer kupelekwa majuu zinakoendeshwa ligi
mama alilala hospitali miezi k+mi na nane
nyumbani miezi ilikuwa ni kama karne
tulimzoea mama baba hakupagawa
alisimama imara j+po mambo hayakuwa sawa kamwe
maisha yalibadilika tukabadilika pia
familia ilipata shida ila baba aliisimamia
ukubwa ulimshika majuk+mu yalishika njia
yalimkaba shingo ila sikuwahi kusikia +n+lia
bahari ikichaf+ka inampima nahodha wa meli
kama ataogopa kufa au ataongoza kweli
lakini si mawimbi samaki waliododosha meli
bali ni rafiki wa karibu wa mama anaitwa mary
mary alimjali baba alimzidi rose
alimzidi rahma alimzidi shosi
alimletea baba kadi aliniletea chopstick
alifua nguo aliosha vyombo na alipika msosi
aliingia mpaka chumbani kwa mdingi
na udhaifu ukaanza yumbisha misingi
mary alimshawishi baba baba akaingia kingi
kwa muda akamsahau mama akapitiwa akamsaliti ah
hamu ya tendo ikawazidi maarifa
kijakazi akazibeba taarifa
miezi kadhaa baada ya mama kupona
akasimulia yote aliyoyaona kama picha
mama akatokwa na machozi
baba akasota kwa magoti
mbele yangu mi mwanae mbele ya wazee
wakunga wa ndoa wenye busara waliobeba koki
huh
mama akapata mashoga wakali
walitoka jangwa la sahara na kalahari
wenye elimu za kutosha na ajenda kali
wakamwambia talaka ukiomba utazipata mali
mama akiwa na chembechembe za hasira
akashawishiwa na wasomi wenye hira
kwa mbali wamezongwa na tamaa za ngawira
akasahau k+msamehe kama ilivyosemwa mila
mama akafungua jarada la talaka
akaandaliwa majeshi waliojipanga kwa karata
baba aligoma kutoa talaka akiomba wamalizie nyumbani sio mahakamani na mama hakutaka
mji ulifahamu kesi iling’ara
yalipambwa magazeti mengi kwa nakala
wanaume washenzi waliongea wapambe
vijiwe vya uswazi waligawana pande ka masihara
mzee hakukataa mwisho akakili kosa
talaka ikaidhinishwa ndoa ikadondoka
baba akapata uchungu likamshukia rungu
kisha mama akaonyeshwa fungu akachota
afya ya mama ya uchumi na mwili vikanawiri
akawa malkia mji ukatabiri
baba akawa kama kifaranga kwenye mvua
bado alimpenda mama na mama hakujua
mama aliitwa superwoman ama soja
aliushinda usaliti aliushinda ugonjwa
baba alimkosa mama kwa starehe ya usiku mmoja
alimpenda mama hivyo k+mpoteza maumivu tosha
washiriki wa biashara walimweka kapuni
akaf+kuzwa kazi asiharibu sura ya kampuni
vikundi vya kina mama walisherekea kombe
dingi aliipoteza kazi akaisogelea pombe
hakuwa sawa kichwani aliishiwa energy
hakukuwa na counseling hakukuwa na remedy
zaidi makala zilizoandikwa na mafeminist
pesa zilimwisha mtaani alifuga enemies
magazeti hayakuandika alivyokuwa hero
yaliandika matusi yaliyomzidi kilo
aliitwa malaya shenzi katili
mwanahizaya mwenye cheti cha ujangili
na yakapiga millions
hakukuwa na vyama vya wanaume k+mtetea baba wakasema ana pepo la uzinzi
ustawi wa maisha yetu ulipotea ghafla
wanasheria wakala na pesa za ushindi
aliumia peke yake dunia ilimweka peku
dhambi ilimwacha uchi hadharani
alifanya mema zaidi ya k+mi hayakutosha awe yesu
ila baya moja aliitwa shetani alizubaa
alizubaa na akashikwa na madoa
alikuwa shujaa ila alishindwa kujiokoa
mwamba wa nyenzo ya katikati ulipoondoka
ilimaanisha ni muda wa safina kudondoka huh
hazikusikika sifa zake njema
machozi hayakusafisha jina lake tena
haiba alizokuwa nazo hazikuvutia kamwe
msongo nao wa mawazo ukamvamia mfalme
aliandika barua ya hadithi yake
akisema kilichomtesa sio dhiki yake
bali ni uzito wa alichokifanya
alijiua kando ya bahari uliokotwa mwili wake
Random Lyrics
- sergei barracuda - žádný limit lyrics
- paraziții - degenerația următoare (video version) lyrics
- brian courtney wilson - all i can say (live) lyrics
- orange cake mix - the days of cherry red lyrics
- gaia (gaia baby) - dauna totala lyrics
- jay nice & ru$h - plate of china lyrics
- lefor - настрій lyrics
- tucker zimmerman - a face that hasn't sold out lyrics
- sister margie - icarus lyrics
- pollmixan - кумир (hero) lyrics