azlyrics.biz
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

dizasta vina – kanisa lyrics

Loading...

@dizasta_vina

kanisa rylics
yoh!
salamu kanisa wako mpendwa katika bwana, katika wana waliotaka kufeli nami nazama, tangu jana uwepo wako haupingiki, kisa una nguvu ya kuwavuta wasiosadiki
sikuhitaji mambo ya kugawana madhehebu, waumini dhaifu wanahama hama kama wehu, ikiwa tangu kale wazazi w-ngu walichanganywa, basi hakika sitahuk-miwa kwa kudanganywa, (kanisa)
sidhani ka’ upo sawa kunibeza, maana hata wewe unapitisha dawa za kulevya, tukianza ku-confess yaliyo nyuma ya pazia, we utachomwa moto alafu mi nitaachwa nakuapia
sitaki kuamini kuwa sadaka au kusifu kwa fasihi, ndio vitanipeleka kwa masihi, kitachonionyesha mbingu ni bidii, ya kutenda mema so sitaki kujua dini ipi ni sahihi, ah!
kanisa unatudanganya kirahisi, nyumba ya mungu ni mioyo yetu nahakiki, kwakuwa saa hizi, jua kali njaa hizi zinafanya ukubali kugeuka taasisi
usinishushe hadhi nikizini, ikiwa unafuga wachungaji wenye dhambi kama mimi, kanisa nakupa pole, nje msafi ndani mchafu naomba tusinyoosheane vidole
kanisa unaniasa, niache kutamani vyeo na wewe unajihusisha na siasa, kama mji wa sodoma ulizikwa na anasa, mwisho wako upo kama hautabadilika sasa
haufanani na meli ya nuhu, unaniomba mchango na kodi nimefeli k-mudu, kanisa unanitapeli kizungu, unanizungusha haunionyeshi kanisa la kweli la mungu
eti manabii wana vyeti, kanisa lina account ya mitandao ya kijamii mpaka benki, wahubiri wanavutana kinguvu, kanisa unajitangaza kutafuta umaarufu?
unapishana na muda hakika, unachojua pekee we ni kufa kuzika, unanishauri nije kwako ndoa ikiyumba kanisa, kichekesho kwamba wewe ndio umeyumba kabisa ah!!
kanisa nilikuja uniongoze, nimpende mungu wewe unaifunza nimwogope, jua kali lilinifunza kukaba nikakupa maisha na cha ajabu haujanifunza chochote
nasikia una pande mbili za sarafu, upande mzuri na upande unaoingia dili mpaka na wafu, na unanifundisha baya haliwi na thawabu, nilikuwa mjinga na sasa nayabashiri majawabu
tunahitaji mafunzo halisia, wakati mbinu zako zimejaa mafumbo na sheria, kanisa tunaishi na wanafki kudadeki, unajifanya rafiki sababu ya ulafi wa chenchi
ikiwa huruma ya jah haina kipimo, basi kati ya wanaoomba msamaha nami nimo, dhambi zako sawa? tumezidiana kimo, mungu aliye hai akuepushie shimo, kanisa huh!
umeshindwa kukidhi, utu unakutoka sababu umeshikwa na dhiki, unasahau lengo unasahau umesimamishwa na sisi, pesa inakuyumbisha nawe unayumbisha misingi
kijiwe chako hakikuniingia akilini, nikafata vijiwe vya pombe vikanitia umasikini, kisa kila aliyenionyesha nia nilimuamini, leo siwaoni wote wameingia mitini
haupo hata kwenye hadhi ya utatu, mungu baba, mwana, roho kisa kazi za uchafu, kanisa hauchezi pasi ni rafu, unaremba altale kuliko hata nafsi za watu
kwa sasa ninahisi una bifu, na taasisi binafsi kwa sababu haukuwa mw-ngalifu, kama ndani yako wanaoishi wadanganyifu, na wanasali hautazalisha watakatifu
kuwa mkweli ni wapi ulipoishindwa nielewe, hiyo siri yako hauwezi ukaificha milele, kama nitachomwa moto wa kukushika ni wewe, nishakusafisha kuliko kujisafisha mwenyewe aah!!
composed by dizasta vina @2016

#singida_finest



Random Lyrics

HOT LYRICS

Loading...