duke & songa - mwanga lyrics
intro:
duke tachez, songa, tamaduni muzik!
[verse i: songa]
yea, songa na duke kazini
mungu nisamehe nafanya rap, hizo __ mpe maskini
sasa mikosi mdosi kazeeka
nacheka, sishuki kama soksi za refa
hatari ni kuota moto sio ndoto
afadhali ni k-mzaa mtoto sio choko
vocal sio ndogo
kama unatunza mazingira, inabidi ukate zogo sio gogo
bongo joto na michosho ya mwili
nakuacha wazi ka kicheche kwenye soko la mwili
kinachotoka kwenye ubongo ni siri
siku hizi sio uchizi, kuokota makopo ni dili
huh, nakupa falsafa za muziki
kwa vyombo vingi ka umezama maktaba ya mpishi
hali ilikikaba kwa dhiki
utabaki njia panda kama barnaba na pipi
hook:
[huu ni mw-nga umefika
kaa pembeni kama una nguvu za giza] x4
[verse ii: songa]
naflow kama fish
natoka tamaduni, hakuna wa ku-flow kama sisi
kila rapper naemkuta juu ya mdundo, namtafuna
hadi mifupa, nina roho kama fisi
njoo kama pimbi
uone jinsi nakukunja, nakurusha mi ni soo kwenye jiji
ukikimbia shoo, mi simo
mwana hara kati ka umeingia choo cha shimo
wanasema najua sana vitu
nimegundua kua mwezi ni kama jua la usiku
hakuna kama mi
wengi vichekesho ka mzee ojwaang na mama kayayii
chunga mapafu, vuta tumbaku
ichunguze afya yako kama umetumwa na udaku
navyotunga na ku-rap tu
wanasema nnalugha inayowavuta kama uga wa smaku
hook:
[huu ni mw-nga umefika
kaa pembeni kama una nguvu za giza] x8
Random Lyrics
- zoo babies - interlude (no tastebuds) lyrics
- karma fields - faint echoes lyrics
- dark polo gang - troppo lyrics
- kaisa - alles ist so hurensohn lyrics
- plusmacher - machen plus lyrics
- zelooperz - isbd lyrics
- yoko ono - coffin car (automatique remix) lyrics
- maxime gervais - underdogs lyrics
- vømmøl spellmannslag - gammel thomas lyrics
- now united - legends lyrics