azlyrics.biz
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

duke & songa - ndege lyrics

Loading...

[verse 1: songa]
wengi wanaoskia zile sauti za ndege
huwa wanahisi ndege anaimba
lakini mi huwa sina mawazo ya kizembe
huwa nahisi labda ni kelele za shida
wamepatwa na wenge, au wanamsiba
au wanahitaji msaada mguu umechomwa na mwiba
au labda wameona mwizi akiiba
na hakuna mlinzi, kwa hiyo wanahitaji mchizi wak-mpiga
pengine labda wameona ndege inapaa
wanashangaa, wanahisi ni jini mwenye pembe kadhaa
muda mwingine wanasali
we utahisi hawalali, wapo tu ndani wanajivinjari
pengine ni msanii anamuita dj
kwakua show haijaanza, wanapiga pa
usije pata mshangao wa kibwege
kaa na tafakari k-mbuka hao ni ndege

hook:
unaweza kuwa unapiga mihayo
lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele
ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege
upande wa pili wa ndege
unaweza kuwa unapiga mihayo
lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele
ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege
upande wa pili wa ndege

[verse 2: songa]
wengi wanaoskia zile sauti za ndege
huwa wanahisi ndege w-n-lia
lakini mi huwa sina mawazo ya kizembe
huwa nakaa chini nafikiria
labda msitu ni mpya na wao wameingia
na hawana ndugu, hawajui wapi watafikia
wanapiga mihayo wengine wanasinzia
kiujumla wamechoka, kwa hiyo skia
kabla ya kusema pima
sijawahi skia ndege wamekamatwa na madawa ya kulevya china
kiafya wazima
na wanakata kiu j-po hawajawahi chimba kisima
mabawa ndio nguzo
ya ndege nami kupitia wao ndio hivi nagawa funzo
sina cha zaidi kwako mzembe
nataka kukuk-mbusha kwamba hao ni ndege

hook:
unaweza kuwa unapiga mihayo
lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele
ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege
upande wa pili wa ndege
unaweza kuwa unapiga mihayo
lakini kiziwi anayekutazama, akahisi tu unapiga kelele
ha, na huu ndio upande wa pili wa ndege
upande wa pili wa ndege x2



Random Lyrics

HOT LYRICS

Loading...