eve bahati - imani lyrics
yesu wakati moja na wanafunzi wake
yesu wakati moja na wanafunzi wake
akawa amewaamuru kufanya miujiza
kuponya magonjwa kutoa mapepo kwa jina lake eeh
kwa bahati mbaya walikuja na habari mbaya wakamwambia
yesu tumetumia jina lako
lakini kuna huyu pepo ambaye hakutoka
tukang’ang’ana kwa muda mrefu
tukitoa huyu pepo
tukitumia jina lako yesu yeyeye
yesu akawaambia ole wenu nyinyi
wenye imani ndogo ole wenu
kuna mambo hayawezi kufanyika pasipo kufunga na kuomba
mwenzangu eeh
katika jina la yesu simama na unyanyuke
katika jina la yesu amini jina lake
katika jina la yesu simama na unyanyuke kwa imani
maana aah
imani ya chembe ya haradali
ndiyo imani inayozaa matunda
imani huitaji mf+ko mzima
unaitaji nini eeeh
imani yako inua imani yako eeeh
ukingoja eti uone ili uamini,ole wako
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
yule akida alimwamini mtumwa wake atapona kwa tamko
la yesu imani yako wewe eeh
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
imani imani inua imani yako weee
wanadamu sisi tuna shida moja
niruhusu nikwambie usaidike
mungu anaweza kukutoa katika shimo
shimoo la matatizo makubwa
shimo ambalo ungeambiwa ungetoka ndani ungelikataa
tena ukamwamini mungu wako akakutoa ndani ya shimo
ukamwamini mungu wako akakusaidia ukasimama
hivi kesho unajaribiwa tu na kitu kidogo
hata lile mungu alikutoa ndani lilikua kubwa
tena unasahau
unaanza kusononeka
mwenzangu k+mbuka lile alilokufanyia
katika jina la yesu simama na unyanyuke
katika jina la yesu amini neno lake
kwamba unaweza yote katika kristo akutiaye nguvu we eyee
imaniii
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
eeh ni umbali gani mungu amekutoa si ulimwamini na akatenda tenda
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
ooh k+mbuka imani husogeza milimani mlima upi unao kuangaisha
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
hatakama ni mlima wa magonjwa milima
ya aina yoyote imani inaweza inaweza husogeza oooh
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
k+mbuka bwana asema usiogope yupo pamoja na wewee
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
kwa imani yako msubiri bwana ushindi wako upo mlangoni mlangoni
imani ya chembe ya haradali ndiyo imani inayozaa matunda
Random Lyrics
- micu prinzz - duet lyrics
- kabirya - stanza lyrics
- albert posis - new beginning lyrics
- bluestaeb & s. fidelity - that's ok lyrics
- sweetheart (rus) - просто (just) lyrics
- frances forever - depression lyrics
- alisa - b.b.w lyrics
- rot rose - my god lyrics
- aquatico zephyrino - balance lyrics
- escualo - alberto lyrics