fid q - bongo hiphop lyrics
bongo hiphop
verse 1:
ulianza wewe.. wakaja waimbaji na wabana pua/
wale mwewe.. franga wawindaji wakatusua/
kwakuwa.. wanajua mshikaji unaishi kwa miko/na zako itikadi.. ziko kimziki na sio mshiko/
kama haileti hela..basi haimake sense.. no sweat kisela mie nikakomaa tu na lako penzi/
sikusound garbage au kuchange suddenly../
mie ni mjeshi so naweza fight savagely/
hiphop ya ukweli.. ukapigwa radioni/sometimes malaika wa heri nao hutembelea motoni/
penzi ni kipofu na anayemuona halioni/ sikuwa na hofu.. mama alinipenda tangu nikiwa tumboni/
i started young.. i made my mother’s womb a drum/
my umblirical chord a guitar.. muhoji aliyenizaa/
bongoflava mzuri kiasi.. hiphop we ndo my queen/ my 1st.. my last & everything in betweenjj
chorus:
mimi na wewe.. tangu long time/ kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame/
cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… bongo hiphop x2
‘
verse 2:
kama kukupenda wewe ni dhambi.. basi shetani yu nami/ na kamwe sintonyea kambi ili niwabambe dukani/
for a million little pieces naweza k-mcon oprah ka james frey/
na watasema sitishi wakati wanaogopa nisitokee/
waufuate mk-mbo huu wa wasomi.. wa midundo na mistari/ ukiwa na nyundo mkononi.. ni rahisi kupigilia msumari/
sio tu bongo.. mpaka ng’ambo hakuna uhuru wa habari/ kuna uhuru wa mwenye chombo.. mitambo na mwenye mali/
kujifanya hawasikii.. haiwasaidii.. wala haiwajengi/ unachosema ni.. kamwe ipp haitompinga mengi/
unawak-mbusha wazazi wa uswazi.. chati ya uteja imeingia/ na mapusha wanauza drugs ili walishe familia/
mbaya.. kuhifadhi fuvu la mtu ndani ya kabati/ mbaya zaidi ni kuwa na ndugu.. halafu kichwa maji/
amka bongo lala.. hiphop sio ufala.. ni lazima uifate/
uaminifu ni kama mshahara.. fanya kazi ili uupate
chorus:
mimi na wewe.. tangu long time/ kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame
cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… bongo hiphop x2
verse 3:
mapenzi ya sikuhizi.. bila kugombana yanakua hayana stimu/
pia ni ruksa kushikana lakini sio kushikiana simu/
inanipa wazimu.. kusikia kimwana haujaachana na hasheem/
na bado mnawasiliana..una mpango wa kuchanganya timu?/
nakupenda hiphop.. ndo maana ninarap ile mbaya/
naspit fire bila hennessy.. au kula kaya/
i want my art to be my legacy.. kabla sijaretire.. waanze nigwaya hawa enemies.. anyways ni hayo tu/
beef huletwa na wivu.. na wivu sio hiphop/
mc nayetaka beef amlete maza ake kwa strip club/
bongo flava ananipima.. kama nimeiva kimasomo/
anagundua mie ni dreamer pia ni believer zaidi ya common/
cha ajabu hunitempt… ili nikuache hiphop/
anaahidi atanipa good s-x.. wewe unanipa true love/
hajui who’s next.. wewe unanipa tu mashavu/
nikipaa.. anaumia.. anatamani nishuke chini/
nami sikutamani ustaa.. ustaa ulinitamani mimi/
nilichohitaji.. ni kuitumia hii sanaa ili nishee na nyinyi/
hii zawadi.. niliyopewa na mpaji ninayemuamini/
mpaji aliyenivika taji ilimradi incharge ni win/
na ninaamini.. kuna muda huongea kwa kupitia mimi/
na hunisamehe ninapokosea.. ni vyema mkanizoea nyinyi/
naweza kuona unachotaka au atakachonionyesha/
nikitoa ngoma.. wanaitaka.. wanaipata.. coz wewe ni special
chorus:
mimi na wewe.. tangu long time/ kabla ya hizi pesa kabla haijaja hii fame/
cha ajabu haujabadilika na upo kwenye mainstream… bongo hiphop x2
Random Lyrics
- vasko atanasoski - sakam lyrics
- magma (2) - lifetime lyrics
- bomba estéreo - soy yo lyrics
- playad - frères d'armes 2 lyrics
- dzy (aka shawn beats) - deshawn187 lyrics
- projota - o mundo é dos loucos lyrics
- russell dickerson - blue tacoma lyrics
- jaromir nohavica - u ns na severu lyrics
- phanto - jamais trop noir lyrics
- c.c.munster - blockade lyrics