azlyrics.biz
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

fid q - propaganda lyrics

Loading...

[intro:]
marco cha+
li

[hook:]
polisi wana support gangsta rap’ ili uhalifu uongezeke
wabana pua kuimba mapenzi je itafanya ukimwi usepe?
media zina promote beef wanadai zinakuza mziki
wadau wana wasanii wabovu, juakali ntatoka vipi

[chorus:]
hizi ni propaganda
usiulize ni nani, ni yupi, saa ngapi? ilikuwaje na nani’ ili iweje?
hizi ni propaganda
utaibiwa ukicheza plan
(yule last king of scotland sio iddi amin wa uganda)
[verse 1:]
machungu unapozimwa ili ufunikwe na asiyeweza
mbaya zaidi wanampa promo lakini kwenye show nina mmeza
hautaki kuwa tatizo sababu unaweza tatuka
huwezi jua wapi ntatoka iwe gizani (?)
wana ficha ili nisione wakati tayari nishajuwa
hamkomi’ igeni nione jinsi msamba mnavyo upasua
hivi una ishi ili ule au una kula ili uishi?
k+mbuka “a small leak will sink a ship”
mazingira hatarishi mabwana afya wana pesa mob
uswazi tunaomba mvua zinyeshe, ili itapishe vyoo
ogopa kua haraka kama unaogopa talaka
na uki+vote in a hurry ujue una produce corruption
maneno yao matamu, midomo yao inanuka
ukipewa usisahau, ukitoa toa’ bila kuk+mbuka
usihofie kupitwa ili mradi muda haukuachi, amini kesho itafika kama ipo ili uipate
tuna chukiana kwasababu tunaogopana
tunaogopana kwasababu hatujajuwana
hatujuwani kwasababu tunatengana
dunia ni nzuri, walimwengu hawana maana

[hook:]
polisi wana support gangsta rap’ ili uhalifu uongezeke
wabana pua kuimba mapenzi je itafanya ukimwi usepe?
media zina promote beef wanadai zinakuza mziki
wadau wana wasanii wabovu, juakali ntatoka vipi
[chorus:]
hizi ni propaganda
usiulize ni nani, ni yupi, saa ngapi? ilikuwaje na nani’ ili iweje?
hizi ni propaganda
utaibiwa ukicheza plan
ah
(yule last king of scotland sio iddi amin wa uganda)

[verse 2:]
polisi huniita mzururaji na wanajua mi ni emcee
kisha hunipa ishara ka wanavuta radi kwa tasbhi
baya lisilo nidhuru ni jema lisilo na faida
nashukuru kote nasikika nnapo toa haya mawaidha
kwanzia kata, tarafa, wilaya, mikoa, hadi ngazi ya taifa
nikifa’ siachi skendo na uhakika nitaacha pengo
kwa hivi vina hata wakulima hujikuta wanameza mbegu
pia ni kama liberation struggle machoni mwa (?)
ukiwa mkali kama marco chali, raia wata feel tu
wajinga ndio hufa kwa wivu, sababu hawako real tu
urafiki sio urafiki usipo changanywa na kazi
mlango sio mlango hadi ufungwe au uachwe wazi
haupaswi k+mwamini muongo hata kama akiongea kweli
ni dhambi kutumia dini kama njia ya kututapeli
wanajiingizia kipato kwa kivuli cha misaada
hawatufunzi tuwe viongozi labda viongozi wa kuwafata
utata huja’ tunapoanza kuwa chunguza
(badala?) ya kuwafata ndipo siri zinapovuja
tunajenga tabia kisha tabia zinatujenga
ukishindwa kujiendesha ujue mwenyewe tu ulipenda
kama umevutiwa na asali ujiandae k+mkwepa nyuki
hauwezi k+mtisha kwa mawe adui aliyeshika bunduki
ni uchunguzi tu wa ki sayansi ambao haukufanikiwa
kama ng’ombe kula nyasi tu halafu anatoa maziwa
[hook:]
polisi wana support gangsta rap’ ili uhalifu uongezeke
wabana pua kuimba mapenzi je itafanya ukimwi usepe?
media zina promote beef wanadai zinakuza mziki
wadau wana wasanii wabovu, juakali ntatoka vipi

[chorus:]
hizi ni propaganda
usiulize ni nani, ni yupi, saa ngapi? ilikuwaje na nani’ ili iweje?
hizi ni propaganda
utaibiwa ukicheza plan
(yule last king of scotland sio iddi amin wa uganda)

Random Lyrics

HOT LYRICS

Loading...