fid q - ripoti za mtaani lyrics
[intro: zahir zorro & fid q]
[drop]
woo…
[drop]
inasikitisha
inahuzunisha, (uh)
inasikitisha
kweli imetokea
[verse 1: fid q ]
maisha safari ambayo tayari imekwisha kwa zake juhudi
alipo kimbilia ni mbali, humchosha akifikiria kurudi
pole pole ‘ndio mwendo, kila akik+mbuka inamuuma
kwanza viliumbwa vidole, binadamu ndio akaunda uma
anaamini ye ni mwema na wabaya mungu hawahitaji
samaki ana mengi ya kusema lakini mdomoni ana maji
muadithihaji akiwa ni mmoja, stori huwaga haikamiliki
msihishereh+sh+, bora mjivishe tu viatu vya huyu binti
aliye mtunza miezi tisa tumboni ndiye aliye mfunza kutambaa
lakini babaake aliye mzaa, alimshauri aache shule ili aolewe
kwasababu mama hana sauti aliona tu bora amuelewe
bora aolewe tu na huyu kijana
j+po hamjaridhia moyoni, kwa kuwa mwanzo ashaujua
haiwezi k+msumbua mwishoni
kadri unavyo mzengua paka, ‘huzidi nyanyua mkia
ghafla akaitamani talaka, akageuka kiruka njia
mwana akagida sumu akafa, ‘alidata baada ya kusikia
demu ashamkomba mkwanja, amesonga kiwanja, amemkimbia
anachukuliwa tu na wajanja, hajui kubana ye huachia
binti hakuacha mlango wazi ili wageni wasigonge sana
hakujua
haya mambo yanaweza k+muharibia usichana
akaonekana
hana mpango ‘mrembo, kwa starehe za ujana
tangu afya yake sio mdebwedo, anakimbiwa tu na mabwana
wa kwanza, alimpata club, ‘binti akafika kikweli
akamvisha mng’aro wa silver mkubwa zaidi ya [?]
siku zikapita ki maisha akaanza kufeli
kwa kuwa uongo aliuzidisha, amejikuta yuko nje ya ukweli
(nje)
[chorus: zahir zorro]
woo…
inasikitisha
(inauma)
inahuzunisha
(inaniuma sana)
inasikitisha
kama kokote imekwama
(kweli imetokea)
lazima niseme
ah
kweli imetokea
lazima niseme
woo…
na hizo ndizo ripoti za mtaani
na hizo ndizo ripoti za mtaani
na hizo ndizo ripoti za mtaani
lazima niseme
[verse 3: fid q]
alipenda kwenda na tarehe, ‘akasahau siku hazilingani
pesa huja na starehe, na matatizo humo humo ndani
hakuna kinacho kauka mapema, ‘zaidi ya machozi
j+po macho hubaki mekundu, na usoni ishara ya majonzi
kizuri ni kizuri, lakini chenye ubora ni bora
kwa bahati nzuri au mbaya, akaja mchimba madini wa [kakora]
akashoboka na huyu binti wa mjini
aliye msafisha macho, akamuhonga gari, nyumba na kila alichokuwa nacho
amesahau alitoa machozi, damu na jasho
kipindi ana hustle, siku si nyingi ana amini atarudi hapo hapo
siku zote adamu hakosi eva wa k+mshawishi
haijalishi maji ni ya moto, lazima ataurudia ubaridi
akipumzishe, kitaota kutu, wakati hii kitu sio ufunguo
namuomba mungu ‘amsitiri zaidi ya mwili wake na nguo
hakutaka kuonekana kama kifaranga cha kuku
kila siku atanyonya kesho ‘wakati maziwa iko huku
kijana akawa mchezaji, ‘zaidi ya ronaldo wa brazil
tisa ukiongeza moja, bado haikamilishi dozen
(?) alio wavisha kofia, wote hawakuwa na vichwa
alicho poteza akihesabu, anahesabu alicho bakiza
[post+chorus: zahir zorro & fid q]
inasikitisha
(inauma)
inahuzunisha
(inaniuma sana)
inasikitisha
kama kokote imekwama
(kweli imetokea)
lazima niseme
ah
kweli imetokea
lazima niseme
ah
kweli imetokea
lazima niseme
ndio
lazima niseme
lazima
lazima niseme
lazima, lazima
(ooh)
ndio
lazima niseme
ndio
Random Lyrics
- xonor - killdozer lyrics
- introvertdame - bad for you lyrics
- mm44 turbo shitpost machine - snippet 10/04/24* lyrics
- anna and vulkan - anni 20 lyrics
- long arm witches - but i loved him lyrics
- lasca pedra & isolas - jerk do rudies flacko lyrics
- ynkeumalice - stars collide (fantasy dream) lyrics
- наша таня (nasha tanie) - чтобы (to) lyrics
- andrenalin - счастье (happiness) lyrics
- bilingual - волк с уолл - стрит lyrics