azlyrics.biz
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

kalamashaka - tafsiri hii lyrics

Loading...

[intro: vigeti]
straight from the mau mau camp (yeah!)
in the red corner… (ahaa!)
muliro, the oteraw
in the blue corner…
kamau, githingithia
and i’m the referee, the mr. vigeti
kalamashaka! (yeah yeah)
anzisha moja mbili
fundisha kiswahili
angusha

[hook: vigeti]
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini

[verse 1: vigeti]
tafsiri
wewe unastahili kunipa nafasi
nitumie swahili
mi nizuru mpaka kila nation
nikitangaza kuwa afrika kuna matata
basi mashaka
wadogo kwa wakubwa huku nasi tunapata
hakika hatuna kichwa wala mkia hapa
akina obobo, kauzi sasa wako kwenye wira
wape hiyo correct [?]
nilishika microphone kila
siku ili niwe kama puff daddy ama yule busta
hakuna tumaini
nadhani nitakuwa ka omondi ama rasta
yaani washa nikiyaweka akilini
sasa nitazuru ruaraka
nipate angalao chupa kadhaa za tusker
ili nisahau hizi taabu zangu
ah! mungu w-ngu
zitaisha lini?
kila siku mimi ninawaza ninakaa
nijipeleke futi sita chini ni balaa
sasa mimi niko na josiah ninawapatia verses shinda bibilia

[hook: vigeti]
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini

[verse 2: kamaa]
nikueleze
vile kule d kama wyclef na phonte si hujaribu
ku-stay alive, vile si hu-survive
’95 tulianza kuroga ili tupate za mboga
sio juju kukoroga, ni muziki kucheza
ili ghetto tuweze toka
tukishaomoka
pick up vijana wa soka
wa timu ya mysa, kabisa
ghetto tutatoka bila kupiga watu tisa
tumaini siku moja chapaa utakuja kuingiza
na utakuwa ukitembea bila kuulizwa
‘kijana unaenda wapi?’
utakuwa ndani ya ‘cedo ukiishia kula happy
najua kwa huu wakati ni ngumu kuamini
ama unashindwa utafika huko lini
kwani kuanzia utotoni umekuwa kule chini
na umaskini umekuwa ni rafiki
utapatwa na riziki

[hook: vigeti]
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini

[verse 3: oteraw]
mabeshte kule ghetto mi huniita al pacino
njaro zangu na squad ya watu k-mi
na veli kama ya jesus
nilitamani njaro za credit card na visas
constantly kwenye corner
nak-mbuka saa mbili usiku nikiona
vile mzee akishikwa koo, balaa
nashindwa nikimbilie nani
jambazi? hapana
polisi? hapana, watanitia pingu hata bila sababu
maisha ni magumu, nilikataa elimu
mama yangu alidhani mimi ni wazimu
siku-lose hope nikaanza ku-drop
lyrics moja kwa moja, pata heshima kama pope
smile, siku zote piga nduru
sababu nimepata lita mbili za kunguru
tafsiri, si siri
wengi toka ghetto wamenawiri

[hook: vigeti]
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini
tafsiri hii, maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii, ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini

tafsiri hii
maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii
ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini

tafsiri hii
maisha kule d ni mazii
mi nalia nikitumia mic
tafsiri hii
ingawa tuko chini bado tuna tumaini
sikiza kwa makini

[outro]
dando, (tafsiri)
kariobangi (tafsiri)
na huruma (tafsiri)
jerusalem (tafsiri)
kila- (tafsiri)
na kule coast (tafsiri)
na kisumu (tafsiri)
tafsiri…



Random Lyrics

HOT LYRICS

Loading...