muzley - asiyefunzwa lyrics
asiyefunzwa lyrics
verse 1
paukwa pakawa kijana mmoja kwa jina la utani walimwita mc pasapasa
kwa utabiri wa hali ya haga alikuwa namba moja kuwafata
mademu wa kitaa wenye hips na rasa
na akipata chenye alitaka haswa angawaacha
juu alipenda sana anasa
vituko vya naswa
akiwa form two chuo akawacha
stress kwa wazazi wake vile walistruggle school fees waipate
wakajaribu juu chini k-mregesha chuo but nothing happened
manake alikuwa haliskii la mwadhini wala la mteka maji msikitini
focus ni ya kupata shilingi
alianza na wizi wa kuku
ili apate hela ya kununua kitu kama nduku
bhangi ikampandisha ngazi akajiona ako tu juu
ya mbuzi kama yeye waliokuwa wakichana matawi
hadi usiku wa manane mida wachawi
hutembea uchi wa mnyama
akataka kilicho mvunguni kama hajainama
design ya kutaka kuokota noti kwa floor kama umesimama
kijiji mzima akajulikana kwa matendo yake mabaya
ikabidi ametorokea mjini kabla hajauawa
hook
asiyefunzwa na mamae hufunzwa na ulimwengu
aliejifunza peke yake atajua risasi sio ndengu
verse 2
jogoo la shamba haliwiki mjini
miezi kama mbili
baada ya kutorokea mjini
wasio mjua walimwona kijana busy
bila kujua alikuwa ashai ingilia zile genge za wizi
kejani wash wash ya mathao
bahasha tao
enemy mkubwa wa makarao
hatambui maskini wala tajiri wote anawapiga bafu chafu
design ya kutaka kutinga goli bila kutingiza wafu
akiwa na ndoto za kuwa punk
siku yenyewe mishoni ilikuwa kuchapia bank
walifika hapo mida ya saa nane adhuhuri na mabonoko
na k-mwamrisha kila mtu juu mikono
kabla wapore ilioskika ni milio ya risasi
polisi wakawaua wote na k-maliza kazi
maisha ya mc pasapasa ikawa imefika kikomo
maana
hook
,
Random Lyrics
- king aiki - bad falling lyrics
- l.o.f.a. entertainment - hit em back lyrics
- donchristian - ss14 lyrics
- sir - faux calme lyrics
- paul kim - 눈 (snow) lyrics
- nessyou - sunsilk lyrics
- kate voegele - it's only life - live acoustic lyrics
- los askis - tiempo al tiempo lyrics
- original flow mastaz - nocturnes lyrics
- dawn richard - spaces lyrics