prof. jay - ndio mzee lyrics
naam ndugu wananchi, mc wenu babu ayubu
ninawaleteeni habari j+po kwa kifupi kuhusiana na huyu mgombea wetu bwana joseph haule
mpeni kura za ndiyo kwasababu yeye ni mpenda watu, ni mpenda amani
na ni mtu mwenye huruma kwa wananchi wote
kwa hivyo basi nawaomba ndugu wananchi, mumpe kula ili aingie
naam basi, hivyo basi ndugu wananchi
eeh, tafadhali namkaribisha mgombea wetu bwana joseph haule
ili aje aweza kuzungumza na wananchi, karibu
okay, okay
naitwa joseph haule, mwana wa msulopo kianzi
nadhani nimeletwa niokoe hiki kizazi
mimi ni mwanasiasa niliyebarikiwa na mungu
nimeletwa kwenu muungwana niwapunguzie machungu
mimi ni mteule kusini mwa jangwa la sahara
ndiyo maana nimetunukiwa cheti cha juu cha utawala
na hekima kuliko mfalme suleiman, msiwe na wasi
na hili nitalidhihirisha pindi mtakaponipa nafasi
actually, nimedhamiria kuwasaidia
taifa lenye nguvu duniani liwe tanzania
jamani, makofi tafadhali basi jamani!
ni mambo madogo tu
nadhani nitarekebisha mkinipa visiku vichache tu
uchumi utapanda ile ghafla bin+vuu
nataka mpaka matonya afundishe chuo kikuu
nchi ya tanzania itang’ara ile kishenzi
na nitahakikisha kila bar+maid anamiliki benzi
si mtafurahi dada zangu jamani? ndiyo
basi endeleeni kunisifu kwa nyimbo na mapambio
nipeni hiyo nafasi jamani, hamwoni hali ni mbaya?
nataka kuigeuza tanzania kama ulaya
cha kwanza nitakachofanya nitafuta umaskini
wanafunzi mkafanyie practical mwezini
kwenye mahospitali nitamwaga dawa kama mchanga
na nitafungua akaunti kwa kila mtoto mchanga
mabomba yatatoa maji na maziwa nchi nzima
watu wa vijijini mtasahau habari za visima
nitafadhili wachawi waweze kutengeneza ndege
kila mtu awe na yake makonda na wapiga debe
si mtafurahi watanzania jamani? ndiyo mzee
si ni kweli nakubalika jamani? ndiyo mzee
basi mimi mkombozi wenu jama, ndiyo mzee
na nitafuta shida zenu zote, ndiyo mzee
hivi ni nanii? ni vijimambo, ndiyo mzee
na vinanikera kweli kweli mimi, ndiyo mzee
basi hali itabadilika sawa? ndiyo mzee
na hatamu tutaishika okay? ndiyo mzee
wafanyakazi wa serikalini nashangaa hamna magari
yaani hata mikweche? he+he! hii ni hatari
ninampango wa kuongeza mishahara iliyo minono
mara mia ya ile ya mwanzo iliyofanya mfanye migomo
nitawapa nyumba nzuri na magari ya kifahari
watu watashangaa mtakapopita kila mahali
mkulima kila mmoja nitampatia trekta
nadhani hiyo kidogo itasaidia kunyanyua sekta
mtauza nafaka zenu bilioni kwa mabilioni
watu midomo wazi kama wamekamatwa ugoni
walimu zawadi zenu oh, nimezificha moyoni
nadhani mtazimia siku mkizitia machoni
we acha tu! mtafurahi nyinyi
ila hapo hapamfai mtu mwingine niwekeni mimi
by the way, polisi wote mi’ nawasifu
jinsi mnavyokwenda sahani moja na wahalifu
sasa kila mmoja nitampatia helikopta
nadhani hiyo wote hapo hamjawahi kuota
raia wa tanzania mtalala milango wazi
in fact, nina uhakika wa kudhibiti ujambazi
nitajenga barabara tano+tano juu na chini
nitajenga k+mbi nyingi sana za starehe baharini
ninaupendo kuliko mshumaa, k+mulikia wenzangu
mtakaoyumba kiuchumi, tutagawana vya kw+ngu
si mtafurahi watanzania jamani? ndiyo mzee
si ni kweli nakubalika jamani? ndiyo mzee
basi mimi mkombozi wenu jama, ndiyo mzee
na nitafuta shida zenu zote, ndiyo mzee
hivi ni nanii? ni vijimambo, ndiyo mzee
na vinanikera kweli kweli mimi, ndiyo mzee
basi hali itabadilika sawa? ndiyo mzee
na hatamu tutaishika okay? ndiyo mzee
ndugu wananchi, kuna mtu ana swali kutoka kwa mgombea?
nauliza hivi, kuna mtu ana swali?
basi ajitokeze ili aweze kuuliza swali
nyie ndugu zangu huyu msimpe uongozi, siyo vizuri
muongo tu, mnafiki na kiburi kimsuli
anaongopea sana! sijui kazaliwa muda gani, alfajiri au alasiri?
au wakati mvua zile, za kipendi kile?
amepita pita school lakini mambo yake si mazuri
wala tusimtetee, atatuangamiza
labda tusubiri kwanza uchaguzi umwekwisha
tumemfuma wenyewe kwa kalumanzila anasafishwa
kalumanzila akamwambia, “ehe, shida yako?
elezea fasta fasta kabla jini haj+panda”
hajakaa vizuri mashetani si yakamuanza!
kamsuk+ma kwa kasi ya kimbunga amejichanja
tulimsikia akisema kwa sauti kubwa ya kukaripia
“waungwana! munisaidie, ndiyo, nitamweleza!”
uongo mtupu babake ameibiwa
waungwana wamempeleka jau mpaka kaibiwa
yupo+hamna gepu na bugzi! amewehuka!
hajatulia huyu mpepeni!
ni sauti iliyosikika kutoka kwa mzee wa pembeni
sijui msaidizi, mganga au mpelelezi
na kwa taarifa yako uongozi hupati ng’o!
labda urudi kwenu uende ukavunje tunguri
na hao waganga wako waeleze hupati kitu apa
hata utoe chapaa
je wananchi mmenisikia? ndiyo mzee
kwa huyu jamaa hatufai, ndiyo mzee
na inafaa k+mchukia, ndiyo mzee
hatumtaki aondoke zake, ndiyo mzee
tusimkubali na maneno yake, ndiyo mzee
tunahakikisha ‘atumchagui, ndiyo mzee
kwasab’ jamaa ni mnafiki, ndiyo mzee
asitufanye tuwe na dhiki, ndiyo mzee
Random Lyrics
- sinan sakić - ko bisere suze lijem lyrics
- süleyman ələsgərov - gəl, qadan alım lyrics
- mr. burn - where my rules apply lyrics
- julia cole - better liar (acoustic) lyrics
- babytron, blp kosher & certified trapper - 3 stooges lyrics
- ak-69 & ¥ellow bucks - noroshi lyrics
- kam prada - fool for you lyrics
- jantho cho - the re-up lyrics
- romero xr - dedans dehors lyrics
- jhart - crash my car lyrics