rapcha - drama freestyle lyrics
tuliambizana tusishike simu za wapenzi tuaminiane
we ulienda kushika ya nini
aliiacha kidogo akaingia bafuni afu akasahau kupiga lock
dah hata mimi ningeitupia jicho naamini
haya ndo mapenzi
ya romeo na julieth , complex na vivian
nenga na nandy (mmmh)
na ndio haya ya pique na shakira aika na nahreel
janja na irene.. (mhhhh!)
mnaanza kwa kukonyezana
mara mnaanza kupendana haya mnaanza tekenyana
ghafla mnaanza kugombana mwisho wake mnapatana
sometimes inashindikana
unachagua ku move on au muwe mnak+mbukana
na wewe kuishi bila ye
ni kama chupa ya chai isiyo na mfuniko
donda lake halishoneki ka umechanwa na gillete
unaisha huku mwenzako anaenjoy
dying slowly like a cigarette
anayekutaka humtaki unaemtaka humpati
nae yuko busy anambembeleza ambae hamtaki
maumivu yanakuua taratibu msaada haupati
wote tunaumia moyo nao kukoma hautaki
mdomo haushindwi kujitetea
kuazimana dera na wigi ndio mwanzo wa umbea
girlfriend wako ana mabest wengi wa kiume unamchekea
watashare hadi na toilet utaelewa
mpenzi wako akikusifia kwa wenzie kuwa we ni muelewa
shtuka kuna namna unachezewa
ndo maana mi kuna muda naelewa
kuna muda sielewi
afu kuna muda sitaki kuelewa
na muda huu umemtext
mchana ulimpigia mara mbili hakushika simu we ukaona fresh
sasahivi kaja online na unaona anapost status
sjui zile missed call hakuziona, dah fresh tu
basi moyo unakuchoma hauna namna
pengine
unajifariji labda hakuziona unapiga nyingine unamkuta bize
bwana!! si ufanye tu ulale
kwani hujui mpenzi wako nae ana mpenzi mwingine!?
afu mkianza mahusiano mnakuaga wakali kama nini
oh nampenda sana jamani wakati mn+z+ni
stress za mapenz zisikufanye ukalewa ya nini
maswala ya moyo usihusishe maini
so ukiona mtu anampiga mkewe
kabla hujahuk+mu kwanza jitahidi sana umuelewe
pili fikiria ingekua ni wewe
tatu fuata yanayokuhusu maana hayo hayakuhusu wewe
na haijaanza leo wala jana
tumeishi tunacheki watu wanaoana wanaachana
sio kwamba hekima hawana
kuna vitu ni vigumu wakuvitatua pekee maulana
wengine wanajiuliza sio bure
rapcha mbona mdogo haya umeyajua vipi hahh too late!
amini kwamba mngejua yote nnayojua
mngejenga misikiti na makanisa zaidi ya shule
unaona wengi wanacheat why!?
asali ni tamu zaidi ya sukari ila haikolei kwenye chai
play part yako piga spana
usije ukaonekana huna maana kwa sababu isiyo na maana
maisha lazma yaendelee
iwe kwa starehe au vilio
hayaishi matukio
uvumilivu ndio unao hitajika
maana msiba hata uwe mzito vipi hatuachi kupika..
ahsante kwa kunisikiliza naitwa rapcha
last king of 90’s
Random Lyrics
- schlussakkord - mit flammen in den augen (part ii) lyrics
- arizera - como é que fica? lyrics
- makalister - semelhante aos acasos e os encontros lyrics
- camouflage - mr. x [demo version] lyrics
- x. ari (pop) - break-point lyrics
- rockstar payso - emerald lyrics
- entropy official music - my life lyrics
- duwap kaine - bluff lyrics
- szymeh (pol) - bongo lyrics
- don toliver - bluetooth (wagyu)* lyrics