raptor el shariff - mwezi mwema lyrics
leo hii ni ya kwanza
tuwe wenye kujipinda
tufanye ano yapenda
na k+mridhi jalia
tumuombeni jalali
mchana pia laili
na kila tunaposwali
atujaalie afia
tufunge bila usiri
tena kwa nyingi sururi
tupate yalo mazuri
mola ‘lotuandalia
tutieni moja nia
kuwa tutajifungia
kwa ikhlasi na nia
na unyenyekevu pia
nayo pia qurani
kwa hima tuisomeni
juzu tukamilisheni
j+po mara wahidia
ni ramadhani ya pili
tumuombeni jalali
atupe nasi sahali
tufunge bila udhia
maaswia tuacheni
kheri nyingi tufanyeni
usiku tuamkeni
ibada kujifanyia
tusipotezeni muda
kufanya yaso faida
bali tufanye ibada
hiyo ndio sawa ndia
ni mwezi wa kuyachuma
mambo mengi yalo mema
basi tufanyeni hima
thawabu kujipatia
pia tushikeni hamu
kuacha yalo haramu
kwani hini ni awamu
ya kutengea tabia
imewadia ya tatu
kuasi tusisubutu
tusafishe nyoyo zetu
tufuate sawa njia
tuchukueni sabuni
nyoyo zetu tuosheni
nyeupе tuzifanyeni
zitatengea tabia
tuwе sana wakarimu
daima tutabasamu
tupendaneni kaumu
na kuswafiana nia
pia sana tutoeni
tuk+mbuke masikini
toa j+po ishirini
au hata moja mia
imewadia ya nne
mema tuamrishane
zaidi tuhimizane
maovu kuyakimbia
na mikono tushikane
pema tuelekezane
wengine tusitukane
na tukajiharibia
msaada tupeane
mazuri tuambiane
katu tusipotoshane
tukaja potea njia
enyi ndugu tupendane
tuloteta tupatane
usiku tuamshane
ibada kujifanyia
pia sana tung’ang’ane
ibadani tushindane
thawabu zipatikane
ziwe mia kwa mamia
leo tano ramadhani
kamba tukaze jamani
tuzameni ibadani
thawabu kujichumia
tuleteni adhkari
usiku pia nahari
tuseme yalo mazuri
maovu kuyakimbia
darasa tusikilize
mambo mema tujifunze
katu damu tusilaze
mazuri kujifanyia
sadaka tutoe sana
vyema kusaidiana
‘tatubariki rabana
‘kifuata sawa njia
ya sita imewasili
shukurani kwa jalali
kuzidi tupa sahali
saumu kujifungia
tuzidi sana kuswali
kwa ikhlasi ya kweli
maovu tuweke mbali
tuzidi kuyakimbia
pia swala za laili
tuamkeni tuswali
ndio mwendo wa rasuli
nao maswahaba pia
tufanye yalo mazuri
tena kwa hamu na ari
maovu tutahadhari
yasije tuharibia
ya sabaa imefika
kwa uwezo wa rabuka
kamba tuzidi kushika
tusije iachilia
tusipoteze wakati
jikoni sana kuketi
kuzipika kaimati
na vyakula ainia
na sana tujitahidi
tuweze kuzifaidi
za ramadhani zawadi
mola ‘lotuandalia
tusikubali kabisa
fadhla nyingi kuzikosa
hivyo tuache mikasa
itayotuharibia
ni ya nane ramadhani
shukurani kwa manani
kututia uzimani
tuna siha na afia
fursa tuitumieni
kuzizidisha imani
na tujirekebisheni
ziwe nzuri tabia
miraa tuiacheni
sigara tusivuteni
nayo pombe tusinyweni
mchana usiku pia
tabia tuache nyuma
zile zisizo njema
tufuate mwendo mwema
mwendo wa wetu nabia
kwa uwezo wa rahimu
ya tisia imetimu
tuifungeni saumu
kwa ilio safi nia
tupunguzeni kulala
tuamkeni laila
na kusimamisha swala
tutubuni sana pia
tuamkeni suhuri
karibu na alfajiri
ndio suna ya bashiri
tusiwe tutapuzia
ya k+mi ni leo hii
basi tufanye bidii
mola tuzidi mtii
tusichoke nawambia
hakika ya mwezi huu
fadhila zipo ni kuu
tusije tukala huu
mema kutojifanyia
tufanye kwa kila hali
aturidhie jalali
na adhabu kali kali
mola ‘tatuepushia
tuzishindeni nafusi
tuyaepuke maasi
tumuombeni qudusi
atuonye sawa ndia
kwa furaha tulianza
sasa k+mi ‘memaliza
basi tusije legeza
kamba tukaachilia
leo ni k+mi na moja
tujizatitini waja
ili tuone natija
mwishoni tukifikia
kwa wingi tukisomeni
kitabu chenye thamani
si kingine qurani
n+z+di kuhimizia
adhkari tusomeni
asubuhi na jioni
nyoyo ‘tapata amani
na pia kufurahia
shukurani kwa jalali
‘mefika k+mi na mbili
tuache lile na hili
tufunge kwa safi nia
kwa safi nia tufunge
pia vyema tujipange
mengi mema tuyachange
mizani kujijazia
ziwe nzito mizani
tufikapo hisabuni
mwisho tungie peponi
tukawe naye nabia
basi tufanyeni hima
tujitahidi kuchuma
mengi mengi yalo mema
sadaka na zaka pia
atujaalie wahabu
qiyama ‘sipate tabu
tuvipokee vitabu
kwa mkono wa kulia
leo ni k+mi na tatu
tusafishe nyoyo zetu
tuitoe yote kutu
turekebishe tabia
mwenendo uwe mzuri
tuzifanye nyingi kheri
adhabu zote na nari
mola ‘tatuepushia
tuzidisheni juhudi
tumuombeni wadudi
sisi sote atuhidi
kwenye ilo sawa njia
k+mi na nne yaumu
ndugu tushikane hamu
kuyaacha ya haramu
halali kuk+mbatia
tuifungeni saumu
kwenye ibada tudumu
tutapata ladha tamu
ya imani nawambia
tuweni na ikhlasi
riya tuseme ni basi
na malipo kwa qudusi
tuwe tutatarajia
leo ni k+mi na tano
tuyaache magombano
kutoleana maneno
na kutukanana pia
tusiweni tutateta
na kuvieneza vita
na kizazi kukita
hizo si njema tabia
tuishi kwa itifaki
tuzitoe zote chuki
upendo uwe wa haki
nyoyo zutafurahia
k+mi na sita ‘mefika
tuzitengeze huluka
nazo radhi za rabuka
tuwe tutajipatia
mwenendo wake hashima
kiigizo chetu chema
tufuate hima hima
hiyo ndiyo sawa njia
Random Lyrics
- yeri yok - suçlu ben değilim lyrics
- billy talent - afraid of heights (demo version) lyrics
- jance - 4 brothers freestyle lyrics
- explosión de iquitos - que tienes tú lyrics
- killa (jpn) - xxx lyrics
- pablo lavins - viva el cometa lyrics
- joni mitchell - song to a seagull (2021 remaster) lyrics
- mxp - kurslos lyrics
- superfly - 愛をこめて花束を (ai wo komete hanataba wo) lyrics
- switchupcb - daydream lyrics