rostam (tz) - kijiwe nongwa lyrics
alikuja kama masii tukamchangia sadaka
tukamwona nabii aliyeshushwa siku ya pasaka
tukamtolea na zaka ili kanisa lijengwe
eeh+eh na bado wakamlaza nabii kifo cha mende
hivi unamk+mbuka babu? babu wa loliondo
ah+ah yule mfugaji mwenye bleach la kikogo
watu wamekufa, watu wamefungwa, watu wamepoteza biashara
sasa umekaribia uchaguzi amerudi chama tawala
vipi dada yetu wa igunga, mmh simwoni udangani
ah mbona ashapata mchumba sio viben 10 wa zamani
yule fundi gereji chawa, si kamateka bibiye
na wamefungua mgahawa, yaani wote mama ntilie
na kuna dem aliyeachiwa mtoto akaolewa na mtoto
akaachana na mtoto akabaki anamlea mtoto
hizi ndoa za mjini bwana, zinasikitisha
eeh maana hufungiwa chumbani na huvunjikia insta
so soka la bongo linakwama wapi? tff maanake nini
tanzania football failure, ndo nacho jua mimi
unamf+kuzaje amunike ili udhaifu wenu umvuge
wakati mlimpeleka mlevi ye akacheze namba ya mkude?
nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero
ukuta tunavunja kwa tindo
wameshapigwa guu wako telo
na kiki za kikolo
majita tushapiga kishindo
hili ni f+gio la chuma
linang’oa visiki
safisha vichaka kwa moto
simba kageuka duma
jangwa halipitiki
ukitufuata umetoa boko
marehemu walimsema mnyonyaji, kwani mziki una maziwa?
sasa mungu kamhitaji na bado hajafanikiwa
hivi unadhani ndani ya mjengo nani ataliziba pengo?
acha maisha yaendelee, jasiri ameumaliza mwendo
aliyeokota almasi mchangani alikuwa miss tanzania
na aliyekuja inunua dukani ni mganda aliyekuwa na nia
ya dhati la pakato akatokea mara mia
akawatumia ila mwamba ni mnyanyasaji wa kijinsia
sa skiza man hii, vipi shem mama ivan?
ah tupo tupo tu ila hatupo ka zamani
nawe vipi kwani, mbona wife simuoni nyumbani
hey chill man, sina majibu deal done
bungeni daily majanga, viongozi wameishiwa mada
hivi mbunge wako wa tanga hoja zake un+z+skiaga?
sa nitazisikiaje? na ana spika mbovu za wana kijiji
ila fundi wao anakuja soon kutoka ubelgiji
nabii tito na dr shika, tayari wamesahauliwa
mwenzao mariamu, biriani anapika anapakuliwa
bongo bwana, ndo nchi inayosupport sana ujinga
utashangaa amber rutty kala shavu ubalozi wa kinga
yaliyosemwa yamesemwa
kazi kwenye mmezoea kutema
wakitaka tuyajenge tena
waambie muda sio rafiki mwema
(yeiye iyee, aah aah iyee)
kusema kweli hatuchoki
na kwenda jela hatuogopi
tutabanana ata kama hapatoshi
hatupindishi ata kwa dumba
nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero
ukuta tunavunja kwa tindo
wameshapigwa guu wako telo
na kiki za kikolo
majita tushapiga kishindo
hili ni f+gio la chuma
linang’oa visiki
safisha vichaka kwa moto
simba kageuka duma
jangwa halipitiki
ukitufuata we toa boko
Random Lyrics
- highlands worship - the earth stood still lyrics
- soyturista - me enamoro lyrics
- teràpia de shock - himne de u.e. fornells lyrics
- jay-z - new york (concept de paris) lyrics
- melodyx_o - jisatsu girls (unfinished) lyrics
- john fischer - only a few lyrics
- avijit pratap singh - transparent forever lyrics
- kelsey lamb - in between time lyrics
- киллми (killmi) - стиль (style) lyrics
- jagger bolek2 - dumb rap song lyrics