slimsal - muda lyrics
sikuwa na ndoto kuishi maisha ya mtaani kwenye kona
j-po siwadharau washakaji wa mtaani kwenye kona
wala sijasahau kutoa tano nikiwaona
kuwatoa tano tano washkaji zangu sioni noma
najua imekuwa kitambo flani washkaji hawajanisoma
wanauliza nimemuachia nani flag la dodoma
wakiuliza nimemuachia nani flag la dodoma
nawauliza mlipatia nani flag la dodoma
najua imekuwa muda sina tena muda wa kupoteza muda
kama nilioupoteza muda nilipokuwa mbele ya muda
muda nilopoteza ndo umenifunza kutunza muda
sina tena muda wa kupoteza muda huu ndo muda
nilipokuwa darasani sikufundishwa kuhusu hela
nilipoingia mtaani nilihisi kama nipo ndani ya jela
nilipopata hela nilitaji tena hela
nilipohitaji hela tena sikuipata tena hela
baba kanifunza kujitegemea bila msaada
mama akanifunza k-mtegemea mungu baba
pia ulimwengu ndio mama ulionilea kama baba
hii dunia ina siku moja we unahesabu siku saba
j-po jana nilikosea njia, lakini leo sina tena hofu ya kupotea
nauthamini muda mchache uliobakia
sababu nyuma kuna muda mwingi uliopotea
sigeuki tena nyuma kuangalia
sababu mbele kuna mengi yanayoningojea
na huu sio muda kunivulia sidiria kisa pene
huu sio muda wa kuchezea mpira na hawa vicheche
huu sio muda wa k-msujudia pusha mwenye kete
huu sio muda wa kusubiri hadi kidole kiwe na pete
huu sio muda k-mlilia shida jakaya kikwete
huu sio muda wa kusubiri huyu aliyefika asepe
huu sio muda wa kutumia akiba aliyokwambia uiweke
ambayo uliitumia kabla ya shida na hali tete
sikuwa na kitu kwa sababu sikuwa na kitu cha kufanya
sikuwa na kitu cha kufanya sababu sikuwa na kitu, hapana
uvivu ni kulala usiku ili kuusubiri mchana
tusipende kutafuta majibu kwa kuulizana
maisha yangu sio kuandika verse na kutoa wimbo
maisha yangu ni kutoka pale nilipokuwa nipo
na kutoka pale nilipokuwepo mpaka hapa nilipo
sio safari ya karatasi kwenda na upepo mzito
Random Lyrics
- m.a.l.c. - bad habits lyrics
- spicyboi thvndx - new phone who dis? lyrics
- safia nolin - dagues lyrics
- buster - itsme lyrics
- naptown's finest - indianapolis star lyrics
- young diamond - my girl lyrics
- norman perry - royal sonesta lyrics
- hammy - ice storm lyrics
- vincenz0 - it wasn't me lyrics
- leboss lynch - adore lyrics