azlyrics.biz
a b c d e f g h i j k l m n o p q r s t u v w x y z 0 1 2 3 4 5 6 7 8 9 #

javan chuna – lugha lyrics

Loading...

verse 1…javan

habari za saa hizi,jamani wazima??/
naitwa said javan kwa majina/
najivunia mbuga za wanyama/
uoto asilia milima mikubwa sana/
pia na lugha mama,ya kiswahili/
nawakilisha ili/
afrika duniani na pote kishamiri/
kama ilivyo pwani ya afrika mashariki/
wageni majirani mngefika anga hizi/
kiswahili ndo sauti makini/
ilitoa tofauti za kidini/
na ubaguzi wa kikabila kati ya wewe na mimi/
natulia bwana najifunza kiswahili/
nakitumia sana na ninatunga mashairi/
hata mniamishe dunia/
kiswahili lugha yangu hata mnivishe gunia/

chorus.adam

nimefika,mataifa mbalimbali/
hesabu kilomita zisizo na idadi/
mimi ni jasiri,siachi asili/
daima sibadiliki na lugha ni kiswahili/
nitaku-enzi/
sababu mimi na wewe ni tangu enzi/
toka jana kesho na muda huu/
kiswahili kiswahili wewe ndo lugha kuu/

verse.2

kiswahili cha mtaa,ama fasaha/
ninaweza kutumia kufikishia hii sanaa/
nikisema vichaa,siaminishi wakosefu wa akili/
ni rejesta na misimu na huku kwetu ni asili/
kiswahili mie wako,popote niendapo/
takutangaza wakusikie,sifa zako wakusifie/
kiswahili cha watu na watu ndo sie/
amasisha askari vitani waende/
vumisha habari vitali maembe/
weka mbwembwe mistari ipende/
kiukweli kiswahili nakuhitaji/
na ndomana kwenye sanaa nakuhifadhi/
watu wa mtaa tunakutaka/
unatufaa tunakufuata/
hata mniamishe dunia/
kiswahili lugha yangu hata mnivishe gunia/

chorus.adam ✖(2)

nimefika,mataifa mbalimbali/
hesabu kilomita zisizo na idadi/
mimi ni jasiri,siachi asili/
daima sibadiliki na lugha ni kiswahili/
nitaku-enzi/
sababu mimi na wewe ni tangu enzi/
toka jana kesho na muda huu/
kiswahili kiswahili wewe ndo lugha kuu/



Random Lyrics

HOT LYRICS

Loading...